Ni kweli inawezekana wanafunzi hao wanahitaji nafasi ya pili kutimiza ndoto zao katika elimu na kuweza kufiti katika ulimwengu wa dijitali.Tatizo kubwa litakalofanya hoja hii isiwe na mafaniio iwapo ikipewa nafasi ni ukweli kwamba watahiniwa wengi wametupa kando na kusahau kabisa mambo ya shule. Nakumbuka enzi zetu tulikuwa tukivunja peni na kuchoma daftari au kugawa vitu hivyo kwa wadogo zetu mara baada ya mtihani wa mwisho.Kama kweli lengo ni kupunguza asilimia ya waliofeli basi inawezekana hoja hii ikafanya kinyume cha fikra za wadau wanaoitoa. Mwanafunzi aliyefeli mtihani alipokuwa shule hawezi kufaulu leo baada ya muda wote huu wa kukaa bila kusoma.
Na ni kwa nini waziri wa sasa ajihuzuru ikiwa jahazi hili amekabidhiwa usukani katikati ya DHORUBA? Kwa nini wadau na wanaharakati hawafikirii haja ya kutafuka chanzo na walioanzisha uozo huu kabla ya kuwahukumu wasio na hatia?.jpg)
Ushauri mzuri ni kuwatafutia waliofeli, si tu wa mwaka jana ila hata wale wa miaka ya nyuma nafasi ya kupata elimu mbadala. Pia bila kusahau kubadilisha mfumo wa kuchagua watu watakaosomea ualimu. Isiwe ilivozoeleka yani kuchagua waliofeli wakasome ualimu na unesi.
.jpg)
No comments: