PHOTOS

DOWNLOAD MP3

VIDEOS

GOSPEL

NEWS

TUTORIALS


First Soja kwa sasa hatakuwa tena kmemba wa kundi la THE EMPIRE na hayuko tena chini ya LEBO hiyo kutokana na makosa aliyoyafanya katika lebo hiyo. Uongozi umebaini kwamba msanii amekosa msimamo thabiti juu ya wapi anatakiwa kutulia. Tangu zamani kumekuwa na uvumu wa taarifa kwamba msanii huyo amekuwa akitanga studio tofauti nje ya lebo kwa madai kwamba anatafuta lebo bado.uvumi huu ulikanushwa na First Soja awali akidai kuwa ni fitina za watu wasiopenda kumwona ndani ya THE EMPIRE.
Hata Hivyo uvumi huo umejidhihilisha baada ya First Soja kuanza kujizungusha na kutafuta visingizio juu ya suala la kisheria la kusainishana mikataba."Dogo alikuja Mwanza kwa lengo la kurekodi ngoma mpya wiki iliyopita. Alipofika alikuta wenzake wote wana mikataba na The Empire,Alipoambiwa swala hilo akaanza uswahili na kujizungusha huku na kule ili amalize ngoma asepe ju kwa juu. Nilipoijua dhamira yake nilisitisha kazi yake ambayo alishakuwa ameingiza verse 1 na chorus mpaka atakaposaini mkataba au laa ajitoe mwenyewe lebo. Kauli yake ikawa ni "ntarudi kusaini baadae na hao mashuhuda wanaohitajika". Hiyo baadae haikufika mpaka leo na akaacha kupokea simu zangu na kunizimia au kuwapa jamaa zake wanijibu" Hayo ni maneno ya producer Mnyambudu.
Kufuatia jambo hilo la dharau na ulimbukeni uongozi wa THE EMPIRE umeamua kumtema First Soja ili awe huru kufanya mambo yake kwa mtindo wake.PIA hataruhusiwa kuzitumia nyimbo alizorekodi chini ya THE EMPIRE zikiwemo "Siyo fea( usiniache)" na "Mapenzi gharama" aliyoimba na Baraka the prince.Hii ikiwemo kuziondoa nyimbo hizo katika media zote na mitandao ya kijamii na BLOGS. Msanii huyo amepewa uhuru wa kuzirudia kuzirekodi track hizo upya popote ila pasipo kuSAMPO track za zamani vinginevyo sheria itachukua time yake dhidi yake.
Hii iwe fundisho kwake na wasanii wengine wenye tamaa za fisi kutaka kila sherehe.Inatisha mtu anapobabaishwa na umaarufu wa mtaani hata kabla ya kutoka. DHARAU hiyo ikifugwa mtu wa hivo hawezi kumheshimu yeyote popote akijulikana bongo nzima.INATISHA....


About mbudutouches

C.E.O at Delta Media Studios, Music engeneer, video director and producer, song writter, graphics designer and music promoter.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Andika maoni


Top