PHOTOS

DOWNLOAD MP3

VIDEOS

GOSPEL

NEWS

TUTORIALS

Dar es Salaam. Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umetaja mambo nane yatakayosababisha Kura ya Maoni isipigwe Aprili 30 kama ilivyotangazwa na Rais Jakaya Kikwete, licha ya kazi ya kuandikisha wananchi kwenye Daftari la Wapigakura kuendelea mkoani Njombe.
Kazi hiyo ya uandikishaji wapigakura ambayo ni muhimu katika mchakato wa Kura ya Maoni ya kupitisha au kukataa Katiba Inayopendekezwa, imekuwa na changamoto nyingi kutokana na kutumia teknolojia ya ‘Biometric Voters Registration’ ambayo hukusanya taarifa za mpigakura, ikiwa ni pamoja na alama za vidole.
Ukawa, ambayo inaundwa na vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD, pia imetaka fedha ambazo zimetengwa na Serikali kwa ajili ya Kura ya Maoni, kupelekwa kwenye uboreshaji wa Daftari la Wapigakura kwa maelezo kuwa uboreshaji unaondelea mkoani Njombe unakabiliwa na changamoto nyingi na kutaka kura ya Maoni kuahirishwa hadi baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Kauli hiyo imekuja siku tatu baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kuanza kuandikisha wakazi wa mji mdogo wa Makambako, ambapo kwa kasoro hizo wakazi wake wamelazimika kuiomba Nec kuongeza maofisa na vitendea kazi ili kuwezesha shughuli hiyo kukamilika ndani ya muda uliopangwa.
Viongozi wa Ukawa, Freeman Mbowe (Chadema), Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Dk Emmanuel Makaidi (NLD) na Mosena Nyambabe (NCCR-Mageuzi), walitoa kauli hiyo jana wakati wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakisisitiza kuwa Serikali inalazimisha mambo isiyoyaweza.
Akitaja sababu hizo, Profesa Lipumba alisema: “Kwanza, Nec haina watumishi wa kufanya kazi ya uandikishaji. Mshauri mwelekezi kutoka Marekani aliishauri tume kuwa inahitaji kuwa na watumishi 10,000 ili kufanikisha uandikishaji nchi nzima na wapewe mafunzo ya kina ya kutumia mashine hizo.”
Alisema watumishi waliopo Makambako ni wachache na wamepewa mafunzo ya siku moja tu, kabla ya kuanza kwa uandikishaji, na wengi wao hawajui kutumia kompyuta wala kamera ambazo ndiyo zinazotumika kuchukua taarifa muhimu.
Alitaja sababu ya pili kuwa ni Nec kukabiliwa na uhaba wa fedha kwa maelezo kuwa ilipewa jukumu la kuboresha Daftari la Wapigakura bila kutengewa fedha za kutosha za kununulia vifaa, kuajiri na kuwapa mafunzo wafanyakazi husika sambamba na kutoa elimu kwa wananchi.
“Tatu, Tume haisemi ukweli juu ya suala zima la uandikishaji. Wamesema watakamilisha kazi Aprili 28 na 30 itafanyika Kura ya Maoni. Nchi ina watu milioni 24 wenye haki ya kupiga kura na haiwezekani wakaandikishwa kwa muda uliobaki,” alisema.
Alisema sababu ya nne ni mashine za BVR kuwa na kasoro nyingi, ikiwamo ya kutotambua alama za vidole gumba vya wananchi ambao wanafanya kazi ngumu, hivyo vidole vyao kuwa na sugu ambao wengi wao ni wakulima, wafugaji na wachimbaji wa madini.
“Sababu ya tano, ni Nec kupuuza ushauri wa mshauri mwelekezi ambaye aliitahadharisha tume hiyo kwamba haiwezekani kutumia mfumo wa BVR kukamilisha kazi kwa wakati kutokana na changamoto zinazoikabili tume hiyo, ikiwamo ya ukosefu wa fedha, uchache wa watumishi, ” alisema.
Akizungumza na Mwananchi mapema wiki hii, mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva alisema ushauri wa mtaalamu huyo ni wa siku nyingi na kwamba alitaka utumike mfumo wa zamani, lakini tume yake imekataa.

About mbudutouches

C.E.O at Delta Media Studios, Music engeneer, video director and producer, song writter, graphics designer and music promoter.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Andika maoni


Top